UMUHIMU WA MABADILIKO KATIKA VIWANGO MBALIMBALI VYA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MUKTADHA WA ISIMUHISTORIA

Authors

  • Zainab Ali Iddi

Abstract

Makala hii inazungumzia umuhimu wa kutathmini mabadiliko ya lugha katika viwango mbalimbali vya lugha. Data za makala hii zimekusanywa uwandani na maktabani. Katika uchambuzi wake makala imetumia nadharia ya Isimuhistoria. Matokeo yanaonesha kwamba kufanya uchunguzi wa kihistoria katika lugha yoyote ni muhimu kwani bila kuangaliwa mabadiliko hayo, lugha haitakuwa na maendeleo. Hivyo, lugha inahitaji kuchunguzwa katika viwango vyote ili kubaini mabadiliko yaliyoingia kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Makala imebaini kwamba lugha ya Kiswahili imepitia mabadiliko mbalimbali katika viwango vyote vya lugha. Baadhi ya mabadiliko hayo ni potevu.

Chakama

Downloads

Published

2022-04-12

Issue

Section

Journals