RIWAYA YA KISWAHILI KAMA KIOO CHA UTAMADUNI WA AFRIKA MASHARIKI: MAENDELEO YANAHUSIKAJE?
Keywords:
Maendeleo, ukoloni, ubepari, pendelevu, riwayaAbstract
Makala haya yanaegemea mtazamo wa kinadharia wa kwamba fasihi huakisi maisha halisi ukiwemo utamaduni. Hivyo basi, riwaya ya Kiswahili ambayo ni zao la wasanii wa Afrika Mashariki, inaweza kuchukuliwa kama kioo cha utamaduni wa kanda hii. Makala haya yanachunguza vipengele vya utamaduni huo ambavyo riwaya teule zinashughulikia, na kujadili ikiwa kwa kufanya hivyo riwaya hizo zinachangia katika maendeleo ya jamii zinazohusika. Hivi ni kwa kuchukulia (kufuatana na nadharia tunayoitumia) kwamba watunzi wa riwaya huwa wamejitolea kuchangia maendeleo ya jamii zao. Kwa hali hii riwaya walizotunga zinaweza kuchukuliwa kama fasihi pendelevu. Data ambayo tutatumia katika uchunguzi huu ni riwaya kumi ambazo zimeteuliwa kimakusudi kuwakilisha awamu muhimu za ukuaji wa utanzu unaohusika na pia maeneo wanakotoka waandishi wake.