KISWAHILI NA MAENDELEO YA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

Authors

  • Ayub Mukhwana

Keywords:

Kiswahili, maendeleo, Jumuia ya Afrika Mashariki, lugha

Abstract

Dhana za maendeleo, hasa kupitia kwa chombo kama lugha, ni tata na telezi. Makala hii imejitokeza na fasiri zake za maendeleo kama dhana na ndizo ambazo kwamo yaliyomo katika makala hii yamejikita. Vyombo mbalimbali vya kiuchumi na kijamii barani Afrika, na hasa Afrika Mashariki, vimerejelewa huku mchango na mafungamano yake na lugha ya Kiswahili katika maendeleo ya Jumuia ya Afrika Mashariki vikijadiliwa. Yaliyomo katika makala hii ni ya kinadharia na vilevile kimatendo ambapo yote yanalenga katika kutoa nafasi ya lugha ya Kiswahili katika maendeleo ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Hitimisho la makala hii ni kuwa, pamoja na changamoto zinazojitokeza, Kiswahili kinao mchango mkubwa katika maendeleo ya kielimu, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia, pamoja na ya kisiasa katika Jumuia ya Afrika Mashariki.

Chakama

Downloads

Published

2022-04-12

Issue

Section

Journals